Psalms 66

Kusifu Mungu Kwa Ajili Ya Wema Wake

(Kwa Mwimbishaji: Wimbo. Zaburi)

1 aMpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote!

2 bImbeni utukufu wa jina lake;
mpeni sifa zake kwa utukufu!

3 cMwambieni Mungu, “Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako!
Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba
adui wananyenyekea mbele zako.

4 dDunia yote yakusujudia,
wanakuimbia wewe sifa,
wanaliimbia sifa jina lako.”


5 eNjooni mwone yale Mungu aliyoyatenda,
mambo ya kutisha aliyoyatenda
miongoni mwa wanadamu!

6 fAlifanya bahari kuwa nchi kavu,
wakapita kati ya maji kwa miguu,
njooni, tumshangilie.

7 gYeye hutawala kwa uwezo wake milele,
macho yake huangalia mataifa yote:
waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake.


8 hEnyi mataifa, msifuni Mungu wetu,
sauti ya sifa yake isikike,

9 iameyahifadhi maisha yetu
na kuizuia miguu yetu kuteleza.

10 jEe Mungu, wewe ulitujaribu,
ukatusafisha kama fedha.

11 kUmetuingiza kwenye nyavu
na umetubebesha mizigo mizito
migongoni mwetu.

12 lUliwaruhusu watu watukalie vichwani,
tulipita kwenye moto na kwenye maji,
lakini ulituleta kwenye nchi
iliyojaa utajiri tele.


13 mNitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa
na kukutimizia nadhiri zangu:

14 nadhiri ambazo midomo yangu iliahidi
na nilizotamka kwa kinywa changu
nilipokuwa katika shida.

15 nNitakutolea dhabihu za wanyama wanono
na sadaka za kondoo dume,
nitakutolea mafahali na mbuzi.


16 oNjooni msikilize ninyi nyote mnaomcha Mungu,
nami niwaambie aliyonitendea.

17 Nilimlilia kwa kinywa changu,
sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu.

18 pKama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu,
Bwana asingekuwa amenisikiliza;

19 qlakini hakika Mungu amenisikiliza
na amesikia sauti yangu katika maombi.

20 rSifa apewe Mungu,
ambaye hakulikataa ombi langu
wala kunizuilia upendo wake!
Copyright information for SwhKC